Kuweka na kutoa fedha
Chunguza njia za kuweka na kutoa fedha haraka na kwa salama ukitumia JustMarkets. Pata njia rahisi za malipo za eneo husika na uhamishaji wa kimataifa kwa kubofya mara moja (1-Click).

Michakato rahisi wa miamala kwa ajili ya kukustarehesha
Tunatoa mfumo wa malipo wa eneo husika na wa kimataifa unaoweza kutumiwa saa 24.

Papo hapo
Tunatoa huduma ya kutoa na kuweka pesa kutoka kwetu papo hapo.¹
Ulinzi wa kutosha
Fedha zako, malipo na data zinalindwa kwa kutumia itifaki mpya zaidi za usalama.
Wastani
Hakuna malipo kwenye kuweka au kutoa fedha na hakuna gharama zilizojificha.²

Usalama kwanza
Tunashughulikia usalama kwa kutumia aina mbalimbali za ulinzi.
Akaunti zilizotengwa
Fedha za wateja wa JustMarkets huhifadhiwa katika akaunti zilizotengwa, jambo ambalo hulinda bajeti yako waziwazi.
Kiwango cha usalama cha PCI DSS
Mfumo wa malipo ya kadi ambao tunashirikiana nao umethibitishwa na PCI DSS.
Miamala salama ya kutoa fedha
Tunatumia utaratibu wa kuthibitisha nenosiri mara moja (OTP) ili kuipa ulinzi wa ziada miamala yote ya kutoa fedha.
Weka pesa kwa kutumia hatua 3 rahisi
Mchakato wa moja kwa moja unaokurahisishia.

Hatua ya 1
Jisajili au ingia kwenye akaunti yako.
Hatua ya 2
Chagua njia ya malipo unayopendelea.
Hatua ya 3
Bofya kitufe cha Kuweka Fedha. Uko tayari!

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi
Kiasi cha chini cha kuweka fedha ni kipi?
- Akaunti ya Standard — Dola 10 za Marekani.
- Akaunti ya Standard Cent — Dola 10 za Marekani.
- Akaunti ya Pro — Dola 200 za Marekani.
- Akaunti ya Raw Spread — Dola 200 za Marekani.
Unawekaje pesa?
Ili kuweka pesa kwa mara ya kwanza, fuata hatua hizi:
- Ingia katika Eneo lako Binafsi (PA).
- Nenda kwenye Fedha -> kitufe cha Kuweka Fedha.
- Chagua akaunti ya biashara ambayo ungependa kuongeza fedha.
- Chagua njia ya malipo unayopendelea kutoka kwenye orodha ya machaguo yanayopatikana. Zingatia tofauti katika kiwango cha chini na cha juu kwa kila muamala na muda wa wastani wa uchakataji.
- Jaza maelezo yako ya malipo (fuata maelekezo na vidokezo vya njia uliyochagua).
- Bainisha kiasi cha fedha inayowekwa katika sehemu ya kiasi. Kiasi unachopaswa kuwa nacho katika akaunti yako ya malipo ukizingatia kiwango cha ubadilishaji fedha kitaonyeshwa katika sehemu ya “Kiasi Kitakachowekwa” (ikiwa inatumika).
- Bofya kitufe cha Kuweka Fedha. Utaelekezwa kwenye ukurasa wa uchakataji wa malipo ambapo unapaswa kujaza fomu ya kuweka fedha na kuthibitisha muamala.
Je, kuna tozo zozote zinazotozwa na JustMarkets kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha?
JustMarkets haitozi tozo zozote kwenye kuweka au kutoa pesa. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba baadhi ya benki na mifumo ya malipo ya kielektroniki (EPS) inaweza kutoza tozo zao za muamala.
Je, ninaweza kutumia akaunti za malipo za ndugu au marafiki zangu kuweka fedha kwenye akaunti?
Katika JustMarkets, tunaupa kipaumbele uwazi na usalama katika miamala yote ya kifedha ili kuhakikisha usalama wa fedha za wateja wetu. Kama sehemu ya uwajibikaji wetu katika kufuata sheria na ulinzi wa mteja, hatuwezi kukubali kutumia akaunti za malipo za wengine kuweka fedha kwenye akaunti.
Unatoaje pesa?
Tembelea tovuti yetu na uingie kwenye Eneo lako Binafsi kwa kutumia utambulisho wako. Fuata hatua hizi:
- Nenda kwenye Fedha -> Kutoa Fedha: Kwenye menyu ya kushoto, chagua Fedha kisha uchague Kutoa Fedha.
- Chagua akaunti yako ya biashara: Chagua akaunti ya biashara ambayo unataka kutoa fedha.
- Chagua Njia ya Kutoa Fedha: Bofya sehemu ya “Njia ya Kutoa Fedha” kisha uchague mojawapo ya njia zinazopendwa zilizoorodheshwa. Hakikisha unajaza maelezo yote muhimu kwa usahihi.
- Thibitisha Kiasi cha Fedha Unazotoa: Kiasi kinachopatikana kwa ajili ya kutolewa kitaonyeshwa chini ya eneo la Kiasi.
- Anzisha Utoaji wa Fedha: Mara baada ya maelezo yote kujazwa, bofya kitufe cha Kutoa Fedha. Idara yetu ya Fedha itashughulikia ombi lako la kutoa fedha.
Mchakato wa utoaji wa fedha unachukua muda gani?
Maombi yote ya kutoa fedha yanashughulikiwa na Idara yetu ya Fedha, ambayo inahakikisha kuwa kila muamala unakaguliwa kwa uangalifu ili kuzuia akaunti yako kufikiwa na wahusika wengine wasioidhinishwa. Mchakato huu unahakikisha usalama wa hali ya juu kwa bajeti yako.
Kumbuka: Katika JustMarkets, tuna mchakato wa kutoa na kuweka fedha kutoka kwetu papo hapo (ndani ya dakika 1). Hata hivyo, ucheleweshwaji kutoka upande wa mtoa huduma unaweza kutokea katika visa fulani.
Mnakubali njia gani za malipo?
JustMarkets hutoa machaguo mengi kutoa fedha. Unaweza kuweka pesa kupitia pochi za kielektroniki (e-wallet), kadi za benki, njia za malipo za eneo husika, WIRE n.k. Angalia njia zote za malipo zinazopatikana hapa.
¹Katika JustMarkets, tuna mchakato wa kutoa na kuweka fedha kutoka kwetu papo hapo (ndani ya dakika 1). Hata hivyo, ucheleweshwaji kutoka upande wa mtoa huduma unaweza kutokea katika visa fulani.
² Mifumo ya malipo iliyochaguliwa inaweza kutoza baadhi ya tozo kutoka upande wao. Inatokea nje ya michakato yetu ya malipo.