Ulinzi wa mteja
JustMarkets ni wakala wa Fedha za Kigeni anayetegemeka ambaye anaaminiwa na mamilioni ya wateja kutoka nchi tofautitofauti. Kwa sasa sisi ni mojawapo ya madalali maarufu zaidi wa Asia na hatusalimu amri kwa washindani katika mikoa mingine.

Kutegemeka
Kutegemeka kwa kampuni ni uwezo wa kukidhi matarajio ya wateja, ubora mzuri wa kazi na huduma.

Uthabiti wa kazi
Kazi yenye matokeo mazuri ya timu ya usimamizi wa hatari ya JustMarkets inahakikisha uthabiti wa kazi za kampuni katika hali yoyote kwenye soko. Hata baada ya uamuzi wa Benki Kuu ya Uswisi kuhusu kufuta kikomo cha juu cha EUR/CHF, jambo ambalo limesababisha matatizo ya kifedha ya madalali wengi wa Fedha za Kigeni kutokana na kubadilikabadilika mno kwa sarafu hizi.
Ukwasi wa benki kubwa zaidi
Uwezo wa kupata fedha wa kampuni ya JustMarkets hutolewa na benki 18 kubwa duniani. Zaidi ya hayo wateja wa kampuni hupata tu bei bora kutokana na kuachiliwa kwa fedha ibadilikebadilike thamani bila kizuizi ambako hutolewa na benki hizi kwa maagizo yenye manufaa zaidi.
Wafanyakazi wenye weledi
Wafanyakazi wa JustMarkets ni wataalamu wenye weledi walio na uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika eneo la kifedha ambao daima wako tayari kusaidia na kutoa msaada unaostahili kwa wateja.
Akaunti zilizotengwa
Fedha za wateja wa JustMarkets ziko kwenye akaunti za benki zilizotengwa, hilo likimaanisha kuwa fedha za JustMarkets na fedha za wateja zimetenganishwa.

Usalama
Kila mteja anapaswa kuwa na uhakika kwamba fedha zake na taarifa zake binafsi zinahifadhiwa salama wakati wa kufanya kazi na kampuni yetu.
Ulinzi wa uhamishaji wa data
Uhamishaji wa data kupitia teknolojia ya kulinda usalama wa uunganishwaji katika intaneti (SSL) na usimbaji fiche wa taarifa husaidia kuzuia kuingiliwa kwa data za mtumiaji na mtu mwingine wakati anapofanya kazi na tovuti, bila kujali mahali alipo.
Ulinzi dhidi ya salio hasi
Kampuni ya JustMarkets hufidia hasara za wateja ambazo zinazidi kiasi cha fedha zilizo kwenye akaunti zao za biashara. Hii inamaanisha kwamba wakati salio hasi linapotokea kwa sababu ya mabadiliko makubwa kwenye soko, litawekwa kuwa sifuri ili kuwalinda wateja dhidi ya hasara zisizotarajiwa.
Kiwango cha usalama wa kimataifa
Taratibu za ndani za kampuni zinategemea kiwango cha usalama cha PCI DSS, ambacho kinatia ndani mbinu tata ya usalama wa habari wa data za wateja.
Mfumo wa seva wa kiwango cha juu
Miundombinu, ambayo inatia ndani seva nyingi, inasaidia mfumo kufanya kazi bila kuingiliwa. Na mpango tata wa kuhifadhi data husaidia kuzuia kupoteza taarifa za wateja (taarifa za kibinafsi, historia ya miamala ya kibiashara, n.k.) katika hali yoyote.
Ulinzi wa kuhifadhi data
Taarifa za watumiaji zinalindwa sio tu wakati wa kuzihamisha kati ya tovuti ya kampuni na kivinjari, tunatoa pia usimbaji fiche wa taarifa zote zilizohifadhiwa ambazo husaidia kuzuia ufikiaji usioidhinishwa wa data za wateja wetu.